China yatoa elimu ya chekecheka bila malipo kwa watoto milioni 12 katika majira ya mpukutiko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2025
China yatoa elimu ya chekecheka bila malipo kwa watoto milioni 12 katika majira ya mpukutiko
Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali ya China (SCIO) ikitoa habari ya sera kuhusu hatua mbalimbali za kuhimiza elimu ya bure ya chekechea, mjini Beijing, China, Agosti 7, 2025. (Picha na Liu Jian/Xinhua)

BEIJING, Agosti 7 (Xinhua) -- Ofisa wa wizara ya Fedha ya China amesema sera ya elimu ya bure ya chekechea nchini China iliyopitishwa kwa kipindi kipindi, itawahusu watoto wote katika mwaka wa mwisho wa shule za chekechea kote nchini, na kuwanufaisha takriban watoto milioni 12 katika muhula wa majira ya mpukutiko mwaka huu.

Naibu waziri wa fedha wa China Bi. Guo Tingting, amesema sera hiyo inatarajiwa kuokoa matumizi ya fedha kwa familia kwa takriban yuan bilioni 20 (kama dola bilioni 2.8 za Kimarekani) katika muhula huu pekee.

Bi. Guo pia amesema ada zilizoondolewa zitalipwa kwa pamoja kati ya serikali kuu na serikali za mitaa, na serikali kuu italipa sehemu kubwa, ambapo mikoa ya kati na magharibi itapata uungaji mkono zaidi. Bi. Guo pia amesema kuwa China itakamilisha sera hiyo kwa wakati ufaao ili kuhakikisha watoto wengi zaidi wanaweza kunufaika.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Renato Lu)

Picha