

Lugha Nyingine
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita kati ya Thailand na Kambodia
Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres anafurahi kuona juhudi zilizofanywa na viongozi wa Kambodia na Thailand katika kusitisha mapigano kati ya nchi hizo mbili, huku akitarajia “pande hizo kuendelea kufanya mazungumzo ili kutatua matatizo yote yaliyopo kati yao”.
Habari zinasema jana tarehe 7 Kambodia na Thailand zilisaini nyaraka za kusitisha vita baada ya kufikia makubaliano katika mkutano maalumu wa Kamati Kuu ya Mambo ya mipakani mwa Kambodia-Thailand. Waziri wa ulinzi wa muda wa Thailand amesema nchi hizo mbili zimekubali kusitisha vita chini ya usimamizi wa mwangalizi aliyetumwa na Umoja wa Nchi za Asia Kusini, pia zimekubali kutoongeza wanajeshi katika eneo la mpakani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma