China yakabidhi shehena mpya ya chakula kwa Zimbabwe

(CRI Online) Agosti 08, 2025

China imekabidhi shehena mpya ya msaada wa chakula kwa Zimbabwe ili kuongeza usalama wa chakula nchini humo baada ya hali ya hewa ya El-Nino iliyotokea mwaka jana kusababisha ukame.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Naibu Waziri wa Huduma za Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii wa Zimbabwe, Mercy Dinha ameishukuru China kwa msaada huo wa chakula unaojumuisha tani 3,000 za mchele na ngano, akisema chakula hicho kitakuwa msaada mkubwa kwa makundi ya raia yaliyo hatarini, ikiwemo familia zinazoongozwa na watoto, watu wenye ulemavu, na wazee.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amesisitiza ahadi ya China ya kuisaidia Zimbabwe kutimiza usalama wa chakula na kupunguza umasikini, akisema msaada huo wa chakula ni sehemu ya majibu ya China kwa ombi la Zimbabwe kwa jamii ya kimataifa la msaada wa chakula kutokana na ukame mkali uliotokea nchini humo mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha