

Lugha Nyingine
Serikali ya DRC yalaani kundi la waasi la M23 kwa kukiuka ahadi ya kusimamisha mapambano
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imelilaumu kundi la waasi la M23 kwa kukiuka ahadi ya kusimamisha vita iliyotolewa katika makubaliano yaliyosainiwa kati ya pande hizo mbili huko Doha, mji mkuu wa Qatar tarehe 19 Julai, na kufanya mashambulizi mengi dhidi ya raia mkoani Kivu Kaskazini yaliyosababisha vifo vya raia wasiopungua 300.
Serikali ya DRC imesema itaanzisha duru mpya ya mazungumzo na Kundi la M23 huko Doha, na pande zinazoshughulikia usuluhishi wa suala hilo zinapaswa kuzingatia kutoheshimiwa kwa utaratibu wa kusimamisha mapambano.
Naye kiongozi wa kundi la M23 Bertrand Bisimwa amesema hawajapata mwaliko wa serikali ya DRC ya kufanya duru mpya ya mazungumzo, na kuishutumu serikali ya DRC kwa kukiuka ahadi kusimamisha mapambano na kuanzisha mashambulizi yaliyosababisha majeruhi ya raia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma