Rais wa Guinea-Bissau ateua Waziri Mkuu mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2025

Rais wa Guinea-Bissau Umaro Embaló alisaini agizo la rais jana, akimfuta kazi Waziri Mkuu wa nchi hiyo Rui Duarte de Barros na kumteua Braima Camara kushika wadhifa huo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ikulu ya Guinea-Bissau, Bw. Camara ataapishwa rasmi ikulu baadaye leo, na atakuwa waziri mkuu wa tatu kuteuliwa na rais Embaló tangu achukue madaraka mwaka wa 2020.

Wachambuzi wanaamini kwamba uteuzi wa Bw. Camara ni jitihada ya kuongeza uzoefu wake mkubwa katika siasa na uchumi ili kuongeza utulivu wa kisiasa na kuhakikisha uendeshaji mzuri wa uchaguzi.

Guinea-Bissau inatarajia kufanya uchaguzi wa rais na Bunge Novemba 23 mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha