

Lugha Nyingine
China yasisitiza kuhimiza ushirikiano wa mapambano dhidi ya ugaidi kati ya Afrika Magharibi na Sahel
(CRI Online) Agosti 08, 2025
Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei amesisitiza kuhimiza ushirikiano wa kikanda kwenye mapambano dhidi ya ugaidi.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja huo kuhusu suala la Magharibi mwa Afrika na Sahel, Balozi Sun amesema China inatarajia Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) itashikilia wazo la usalama wa pamoja, kushirikisha kila nchi ya kanda hiyo kwenye ushirikiano wa mapambano dhidi ya ugaidi, na kuimarishia uratibu na mifumo ya sehemu nyingine dhidi ya ugaidi.
Pia Balozi Sun amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza msaada zaidi na kuzisaidia nchi za kanda hiyo kuimarisha ujenzi wa uwezo wao wa kupambana na ugaidi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma