

Lugha Nyingine
Ofisi ya UM nchini Kenya yaongeza majengo kwa ajili ya mashirika mapya
(CRI Online) Agosti 08, 2025
Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Kenya (UNON) inaongeza majengo mapya ili kuwezesha mashirika mapya ya Umoja huo na Ofisi zake za kikanda na dunia ambazo zinahamishia operesheni zao nchini Kenya.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana jijini Nairobi, UNON imesema mradi wa ujenzi katika ofisi hizo unaogharimu dola milioni 340 za kimarekani unaendelea, ikiwa ni uwekezaji mkubwa zaidi uliofanywa na Sekretariet ya Umoja wa Mataifa barani Afrika.
Mradi huo ni pamoja na ukarabati wa majengo 10 yaliyojengwa wakati Mradi wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa ulipoanzishwa mwaka 1972 na ukarabati wa jengo la ofisi lililojengwa kati ya mwaka 1980 na 2010.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma