

Lugha Nyingine
Wahudumu wa afya wa Afrika Kusini waandamana kupinga hatua ya Israel ya kutumia njaa kuwa silaha huko Gaza
![]() |
Wahudumu wa afya mjini Cape Town, Afrika Kusini wanaandamana kupinga kitendo cha Israel kufanya njaa kuwa silaha huko Gaza, Agosti 7, 2025. (Picha na Shakirah Thebus/Xinhua) |
CAPE TOWN, Agosti 7 (Xinhua) -- Wafanyakazi wa sekta ya afya wa Afrika Kusini kutoka hospitali za umma na kibinafsi Alhamisi waliandamana kupinga hatua ya Israel ya kufanya njaa kuwa silaha.
Katika Mkoa wa Cape Magharibi, maandamano yalifanyika kwenye sehemu karibu na vituo 10, huku maandamano mengine yakipangwa kufanyika katika Mkoa wa Gauteng.
Mjumbe wa jumuiya ya wafanyakazi wa Huduma za Afya wa Afrika Kusini wanaouunga mkono Palestina, Feroza Armien, amesema kupitia maandamano yaliyoratibiwa wakati wa chakula cha mchana kote nchini Afrika Ksuini, wafanyakazi wa afya wanatuma ujumbe kuwa “mauaji ya kimbari yanatokea, na ni lazima kulaaniwa”.
Pia amesema, “Kufanya huduma za afya kuwa silaha ni jambo la mauaji ya kimbari, na hiyo ni kinyume kabisa na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Hospitali na wafanyakazi wa afya wanalindwa kabisa katika maeneo ya vita, bado Israel inawaua wafanyakazi wa afya -- kuwaua, kuwalenga, kuwajeruhi, kuwatesa, kuwateka nyara, na kupiga mobomu dhidi ya hospitali. Hakuna huduma ya afya inayopatikana."
Ameongeza kuwa, wakiwa ni wataalamu wa afya, hawawezi kukaa kimya wakati kazi zao zinatishiwa kabisa na zinatumika kuua badala ya kuokoa maisha, na kazi zao zinatakiwa kusimamia hali hii.
Armien amesema kitu kinachotumika hivi karibuni zaidi kwenye mauaji haya ya kimbari ni njaa. Amesema, "akina mama hawawezi kutoa maziwa kwa sababu wana utapiamlo ... Watoto wanakufa; akina mama wanakufa. Njaa ni kifo cha polepole, cha uchungu na cha hila."
Kwa mujibu wa idara ya upangaji wa viwango vya usalama wa chakula, hali ya Gaza imefikia kiwango kibaya zaidi cha "ngazi ya 5: Njaa/Janga”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma