China yafanya mazoezi ya kwanza ya gwaride la kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi dhidi ya uvamizi wa Japan na ufashisti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 11, 2025
China yafanya mazoezi ya kwanza ya gwaride la kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi dhidi ya uvamizi wa Japan na ufashisti
(Picha iliyopigwa toka kwenye video)

BEIJING, Agosti 10 (Xinhua) -- Mazoezi ya kwanza ya jumla ya gwaride la kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi uliopatikana katika vita vya watu wa China vya kupambana na uvamizi wa Japan na Vita vya dunia vya kupinga ufashisti yalikamilika jumapili Mjini Beijing.

Kituo cha habari cha shughuli ya kumbukumbu hiyo kimesema, mazoezi hayo yaliyofanyika kuanzia usiku wa Jumamosi hadi alfajiri ya Jumapili kwenye uwanja wa Tian'anmen, yalikuwa na washiriki 22,000, ikiwa ni pamoja na wanaoshiriki kwenye mazoezi na wafanyakazi wanaotoa msaada kwenye eneo la mazoezi.

Waandaaji wamesema mazoezi hayo yanahusu vipengele muhimu vya gwaride na ni majaribio kuhusu upangaji, vifaa na utoaji wa amri. Mkusanyiko huo utakaojumuisha gwaride, umepangwa kufanyika asubuhi ya Septemba 3 katika uwanja wa Tian'anmen.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha