Makampuni ya utengenezaji magari ya Ujerumani yakumbwa na kodi Marekani, yazingatia ushirikiano wa China na Umoja wa Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 11, 2025
Makampuni ya utengenezaji magari ya Ujerumani yakumbwa na kodi Marekani, yazingatia ushirikiano wa China na Umoja wa Ulaya
Picha hii inaonyesha banda la kampuni Mercedes-Benz ya Ujerumani kwenye maonyesho ya magari yaliyofanyika kwenye kituo cha mikutanoi na maoneysho cha Singapore, Januari 9, 2025. (Xinhua/Then Chih Wey)

BERLIN, Agosti 10 (Xinhua) – Kuanzia mwezi Aprili, wakati Marekani ilipoongeza kodi kwa kiasi kubwa kwa magari yanayoagizwa kutoka Umoja wa Ulaya, sekta ya magari barani Ulaya imekumbwa na pigo kubwa, na kufanya faida ya makampuni makubwa yanayotengeneza magari nchini Ujerumani kupungua kwa kiasi kikubwa, na kuyalazimu makampuni hayo kutafuta fursa zaidi barani Asia.

Makubaliano ya hivi karibuni kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya yalipunguza kodi kutoka asilimia 25 hadi asilimia 15, na kupunguza mvutano kiasi, lakini wataalamu wametahadharisha kuwa hatua hiyo ni ya muda mfupi, kwani gharama za mauzo ya nje na kukosekana na uhakika wa kisera kunaendelea kutatiza sekta ya viwanda ya Ujerumani na kuondoa imani ya wateja kwenye sekta hiyo.

Makampuni makubwa matatu ya utengenezaji wa magari ya Ujerumani BMW, Mercedes-Benz na Volkswagen, yameshuhudia kupungua kwa kasi kwa faida katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, na sababu ya kupungua kwa faida ni kodi ya Marekani. Kuporomoka kwa mapato kunakoyakabili makampuni hayo sio tu kunatokana na sababu za muda mfupi za ushuru, lakini pia kutokana na changamoto nyingi za kimuundo.

Hatua za kodi zinazochukuliwa na Marekani zinaathiri mnyororo wa usambazaji, huku nchi hiyo ikitoza kodi ya asilimia 50 kwa chuma, aluminium na vitu vingine vinavyoagizwa kutoka nje, hali inayofanya wasambazaji wa bidhaa kuhamishia gharama zinazoongezeka kwa wazalishaji, na hivyo kupunguza zaidi faida yao.

Wakati hali ya kutokuwa na uhakika ikiendelea kuwepo na kubadilika kwa sera za biashara katika masoko ya Marekani na Ulaya, makampuni kadhaa ya Ujerumani yanaangalia zaidi soko la China, ambako kuna utulivu na makadirio yaliyo wazi kuhusu ukuaji wa uchumi. Kupitia uzalishaji wa ndani, ushirikiano wa teknolojia na uwekezaji, makampuni ya magari ya Ujerumani yanatafuta nafasi zaidi barani Asia na kuharakisha mabadiliko ya muundo wake.

Ofisa mkuu wa mambo ya fedha na uendeshaji wa kampuni ya Volkswagen Bw. Arno Antlitz, hivi karibuni alieleza imani yake kubwa juu ya kupanua majukwaa ya ushirikiano katika kutengeneza betri kwenye soko la China. Kampuni ya BMW pia imetangaza ushirikiano na kampuni ya Momenta ambayo ni kampuni ya teknolojia ya China kwenye kuendeleza mifumo ya kizazi kijacho ya kuwasaidia madereva iliyoundwa kwa watumiaji wa China.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha