

Lugha Nyingine
China iko tayari kwa uvumbuzi zaidi wa roboti za binadamu na matumizi yake kibiashara
![]() |
Roboti za ndondi zikionekana kwenye Maonyesho ya Roboti ya Dunia 2025 (WRC) mjini Beijing, China, Agosti 8, 2025. (Xinhua/Xie Han) |
BEIJING, Agosti 11 (Xinhua) -- Roboti ambazo si kama tu zinaweza kukimbia na kucheza soka lakini pia zinaweza kupanga vipuri vidogovidogo na kuviunganisha, na hata kucheza mchezo wa Mahjong, kupiga piano na kutunga muziki, zilikuwa ndoto tu ya hadithi za kisayansi, lakini sasa roboti hizo zinaweza kuonekana katika mazingira halisi yanayoendelea kwenye Mkutano wa Robot wa Beijing (WRC World)
Mkutano wa Robot wa Beijing 2025 unaonesha teknolojia ya akili bandia inayoendelea kukua kwa kasi, huku roboti za binadamu zikiwa kivutio kikubwa, zikionyesha maendeleo makubwa yaliyopatikana duniani na hasa nchini China, huku maonyesho hayo yakitumika kuangazia matumizi ya kibiashara ya roboti hizo.
Maonyesho hayo ya Robot ya Beijing yanayofanyika kwa siku tano yalifunguliwa Ijumaa yakiwa na kauli mbiu ya “Kuzifanya Roboti Kuwa za kisasa, Kuzifanya Roboti za Binadamu Kuwa na Akili Zaidi." Maonyesho yanahusisha mikutano, maonyesho, mashindano na shughuli ya mawasiliano mitandaoni, huku kukiwa na zaidi ya kampuni 200 za roboti kutoka duniani kote zikiwasilisha ubunifu wao wa hivi karibuni.
Washiriki wa maonyesho hayo ya Beijing wanaonesha roboti za binadamu za hivi karibuni zaidi pamoja na aina nyingine za roboti, kama roboti zenye magurudumu, roboti shirikishi, na roboti za mbwa, pamoja na miundo mipya ya akili bandia iliyobuniwa.
Ubunifu wa China kwenye teknolojia ya akili bandia iliyojumuishwa kwenye roboti hiyo, imewezeshwa na maendeleo thabiti ya sekta ya roboti. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa kwenye mkutano huo, mwaka 2024 sekta ya roboti ya China iliingiza mapato ya karibu yuan bilioni 240 (sawa na dola bilioni 33.4 za Kimarekani).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma