

Lugha Nyingine
Rais wa Zimbabwe ahimiza uungaji mkono wa kitaifa katika Siku ya Mashujaa (3)
![]() |
Watu wakiwa kwenye maadhimisho ya 45 ya Siku ya Mashujaa mjini Harare, Zimbabwe, Agosti 11, 2025. (Picha na Shaun Jusa/Xinhua) |
HARARE, Agosti 11 (Xinhua) -- Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amewataka wananchi kuunga mkono maendeleo ya nchi kwa heshima ya mashujaa wa nchi hiyo walioaga dunia wakati wa mapambano ya ukombozi, alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za 45 za Siku ya Mashujaa mjini Harare, Zimbabwe.
Rais Mnangagwa amesema ili kukumbuka daima milele kujitolea kwa mashujaa waliopoteza maisha yao wakati wa mapambano ya ukombozi dhidi ya utawala wa kikoloni, serikali ya Zimbabwe inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya uchumi katika nchi nzima kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wa Zimbabwe. Bwana Mnangagwa amesema, uhuru wa mwaka 1980 ulileta uhuru wa kisiasa, wakati mapambano ya uchumi yanaendelea, na ili kuwaheshimu waliojitoa mhanga kwa ajili ya ukombozi wa Zimbabwe, wananchi wote wanapaswa kuwa na nafasi sawa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa nchi.
Siku ya mashujaa ni sikukuu ya umma nchini Zimbabwe, ambayo inaadhimishwa Jumatatu ya pili ya Agosti kila mwaka ili kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliokufa kwenye mapambano ya kupigania uhuru.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma