

Lugha Nyingine
China yaanzisha kampeni kwenye mtandao wa Internet kuonyesha mvuto wa utamaduni na maendeleo ya mji wa Tianjin
Shughuli inayofanyika kwenye mtandao wa internet ilianza Agosti 9, 2025 katika mji wa Tianjin uliopo kaskazini mwa China, ili kuonyesha mvuto wa kipekee wa utamaduni wa mji huo, maendeleo yake, uwazi na ushirikishwaji wake kabla ya mkutano ujao wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).
Kati ya watu walioshiriki kwenye hafla ya kuanzishwa kwa shughuli hiyo, wakiwemo naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati Kuu ya mambo ya Mtandao wa Internet (CCAC) na Idara ya Usimamizi wa Mtandao wa Internet ya China Bw. Niu Yibing, naibu mhariri mkuu wa People's Daily Bw. Xu Lijing, mjumbe wa kudumu wa Kamati ya Chama cha CPC ya Mji wa Tianjin na mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati ya CPC ya mji wa Tianjin Bw. Shen Lei, na mkurugenzi wa Ofisi ya Sera na Kanuni ya Idara ya Kitaifa ya Urithi wa Utamaduni (NCHA) Bw. Jin Ruiguo.
Maonyesho kadhaa yalifanyika ili kuonyesha utamaduni wa kipekee wa Tianjin, maendeleo ya kisasa na habari kuhusu maendeleo ya hali ya juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma