

Lugha Nyingine
Roboti ya paa wa Tibet yaungana na kundi la paa (2)
![]() |
Mtaalamu akiifanyia majaribio roboti ya paa wa Tibet katika mji wa Golmud, Mkoani Qinghai China, Mei 22, 2025. (Xinhua/Liu Silu) |
XINING, Agosti 12 (Xinhua) -- Kila alasiri inapoingia, jua linaanza kuleta joto kwenye Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, na kufanya wakati huo kuwa wakati wa kilele kwa Paa wa Tibet kutafuta chakula.
Mnyama mkubwa kidogo anasimama juu ya nyasi. Tofauti na wanyama wengine, ambao wameinamisha vichwa vyao ili kula, "paa" huyu anainua kichwa chake, akisonga mbele kwa uangalifu huku akielekea kundi la paa wengine.
Ni Roboti ya Paa, ambaye, kwa mbali anaonekana na kufanana na paa halisi walio karibu, wanaofanana kwa rangi, manyoya na umbo la mwili. Lakini ukimsogelea kwa karibu, unaweza kuona kamera ndogo, iliyofichwa chini ya macho yake.
Roboti hiyo ilifanyiwa majaribio mwishoni mwa mwezi Julai huko Hoh Xil, eneo lenye mwinuko wa wastani wa zaidi ya mita 4,600 kutoka usawa wa bahari. Mazingira ya eneo hilo ni ya baridi na hayana oksijeni ya kutosha, na kufanya iwe vigumu kwa binadamu kuishi huko. Wakati huo huo, eneo hilo linafahamika kuwa ni “dola ya wanyama” kutokana na kuwa na wanyamapori wengi.
Aina adimu za huko, wakiwemo Paa wa Tibet, hutumika kama kiashiria muhimu cha kiekolojia cha Uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet.
Wanasayansi wanasema Roboti ya Paa wa Tibet imeweza kushinda vikwazo vilivyowekwa kuhusu umbali ambao binadamu wanaweza kutazama wanyamapori. Inaweza kutoa picha sahihi zaidi, za kuaminika na data kwa ajili ya utafiti wa tabia ya Paa wa Tibet nchini China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma