

Lugha Nyingine
China Kusonga Mbele | Sikiliza midundo ya ngoma na simulizi za historia ya miaka elfu ya Mji Mkongwe wa Kuqa (4)
![]() |
Wakazi na watalii wakicheza ngoma pamoja kwenye kichochoro cha Menbaza cha mji mkongwe wa Kuqa. (Tang Song/People’s Daily Online) |
Wakati usiku unapoanza, taa zinawasha taratibu kwenye mtaa wa Resitan katika mji wa Kuqa wa Eneo la Aksu la Xinjiang, China. Wakati huo midundo ya ngoma ya mkononi na muziki uliopigwa kwa vinanda vya Dutar vinasikika kutoka vichochoro mtaani humo, huku harufu nzuri ya mkate wa naan na tuni ya Muqam vikichangamsha kwa pamoja, hali ambayo inawavutia watalii wengi kutembelea huko.
Mji wa Kuqa, ukiwa mji uliojaa "utamaduni wa Kucha" kwenye Njia ya Hariri, umejenga upya eneo lake kongwe kwa kupitia mradi wa "Urithi wa Utamaduni Usioshikika Waingia Vichochoroni". Kwa sasa mji huo ni kama jumba wazi la makumbusho la kuonesha utamaduni wa aina mbalimbali, ukivutia watalii wa sehemu mbalimbali kuja kujionea utamaduni wa Kucha.
Kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu, mji wa Kuqa umepokea watalii wa ndani kwa mara milioni 7.14 , idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 47.97 kuliko kipindi kama hicho mwaka uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma