

Lugha Nyingine
Michezo ya Roboti za binadamu ya Dunia ya 2025 yaonyesha teknolojia za kisasa (2)
BEIJING, Agosti 14 (Xinhua) -- Michezo ya roboti za binadamu ya dunia ya mwaka 2025 ilianza Alhamisi mjini Beijing, ikionyesha mafanikio ya hali ya juu ya roboti zenye umbo la binadamu katika kufanya maamuzi kwa akili na kufanya vitendo mbalimbali vya kushirikiana.
Michezo hiyo inashirikisha timu 280 kutoka nchi 16 zikiwemo Marekani, Ujerumani na Italia zikishindana kuanzia Ijumaa hadi Jumapili kwenye uwanja wa kitaifa wa michezo ya kuteleza. Washindani watashiriki katika michezo 26 tofauti, inayojumuisha changamoto kama vile kukimbia, kuruka kwa mbali, kufanya mazoezi ya kawaida na kucheza mpira wa miguu, pamoja na kazi zinazotegemea ujuzi kama vile kusogeza vifaa, kupanga dawa na kufanya usafishaji katika hali tofauti.
Ofisa wa idara ya Uchumi na Teknolojia ya Habari ya Beijing, Li Yechuan, amesema mashindano hayo yamepangwa kwa mujibu wa utaratibu wa mashindano ya michezo ya binadamu, ili kuonyesha maendeleo ya hivi karibuni na uwezo wa matumizi ya roboti za binadamu kupitia "majaribio kali."
Mashindano hayo ya michezo ni sehemu ya Mkutano wa Roboti wa Dunia wa mwaka 2025, uliofunguliwa Agosti 8 chini ya kaulimbiu ya “Kufanya Roboti Kuwa na Akili Zaidi”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma