Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2025
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa

Reli ya Harbin-Qiqihar, ambayo ni reli ya kwanza ya kasi ya mkoani Heilongjiang, kutoka mji Harbin hadi mji Qiqihar, ilianza kufanya kazi tarehe 17 Agosti 2015, na kuwa reli ya kwanza ya aina hiyo kuwepo katika sehemu ya kaskazini zaidi mwa China.

Jumapili iliyopita reli ya Harbin-Qiqihar ilitimiza miaka 10 tangu kuanza kazi. Katika muongo mmoja uliopita, treni za kasi kwenye reli hiyo zimesafiri kwa usalama kwa zaidi ya kilomita milioni 81.89 na kusafirisha zaidi ya abiria milioni 100.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha