Michezo ya roboti za binadamu ya China yaonyesha uvumbuzi wa teknolojia ya kimataifa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2025
Michezo ya roboti za binadamu ya China yaonyesha uvumbuzi wa teknolojia ya kimataifa
Roboti za binadamu zinashindana kwenye mchezo wa soka wachezaji watatu kwa watatu kwenye Michezo ya Roboti ya Dunia ya 2025, mjini Beijing, China, Agosti 15, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

Kwenye Michezo ya Roboti za binadamu ya Dunia ya 2025, ambayo ni michezo ya kwanza ya aina hiyo duniani iliyomalizika Jumapili mjini Beijing, timu ya Tsinghua Hephaestus ilipata ushindi kwenye mechi ya roboti ya wachezaji watano kila upande, ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu, na kuziwashinda timu ya pamoja ya HTWK Robots ya Ujerumani na Nao Devils kutwaa ubingwa. Timu ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha China ya Mountain & Sea, pia iliishinda timu ya Sweaty kutoka Ujerumani kwenye mchezo wa fainali ya soka ya wachezaji watatu kila upande.

Michezo ya mashindano ya roboti ilianza Alhamisi ikishirikisha timu 280 kutoka nchi 16 zikishindana katika mashindano ya michezo 26, pamoja na mashindano katika maonyesho, na mashindano ya uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye utatanishi. Mashindano haya ya majaribio kwa madini, chipu na maheshabu yalikuwa na maonyesho kwa ajili ya umma na kuwa jukwaa la kuonyeshana teknolojia ya akili bandia linaloibuka inayowakilishwa na roboti za binadamu.

Mashindano hayo yalijumuisha michezo kama vile mbio za meta 100, 400, na 1500, kuruka kwa kusimama, mazoezi huru jimnastiki na soka. Maonyesho hayo yaliangazia uwezo wa roboti moja moja na vikundi, pamoja na wushu, huku zikifanya shughuli nyingine katika hali iliyoiga mazingira ya hali halisi katika viwanda, hospitali na hoteli. Kwa pamoja michezo hii ilitumika kama jaribio la mwisho kwenye mashindano ya roboti za binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha