Habari katika picha: Mrithi wa ufundi wa ushonaji wa nguo za jadi wa Lhasa mkoani Xizang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 19, 2025
Habari katika picha: Mrithi wa ufundi wa ushonaji wa nguo za jadi wa Lhasa mkoani Xizang, China
Losang Monlam akiwa mbele ya nguo za jadi za kitibet katika shule ya sanaa za jadi za kazi ya mikono ya Sholdo Pal huko Lhasa, kusini-magharibi mwa Mkoa wa Xizang, China, Agosti 15, 2025. (Xinhua/Jigme Dorje)

Mavazi ya jadi ya kiibet, baada ya mabadiliko na maendeleo ya karne kadhaa iliyopita, yamekuwa na mitindo na sifa za kipekee. Likiwa ni moja ya aina kuu ya nguo za jadi za kitibet, vazi la Lhasa linajitofautiana na nguo nyingine za jadi za kitibet kwa kuwa na sifa wazi kama vile kiuno kikubwa, mikono mirefu na safu nyingi za mapambo, ambazo sio tu zinaonyesha mvuto wa watu wa Tibet, bali pia zinahusiana kwa karibu na mazingira yao ya maisha na mtindo wa maisha. Mwaka 2018, vazi la Lhasa liliorodheshwa kama moja ya urithi wa jadi usioshikika wa Mkoa wa Xizang.

Katika shule ya sanaa za jadi za kazi ya mikono ya Sholdo Pal, Losang Monlam anawaongoza wanafunzi wake kufanya ushonaji wa mavazi ya Lhasa. Losang Monlam alizaliwa mwaka 1965 katika Wilaya ya Baxoi ya Qamdo, na alianza kujifunza ushonaji alipokuwa na umri wa miaka 13. Mnamo 1983, alikwenda Lhasa kusomea utengenezaji wa mavazi. Alisema,“Wakati huo, mavazi ya Tibet yalikosa mvuto kutokana na mitindo na rangi.” Baadaye alikuwa mwalimu katika shule ya sanaa za kazi ya mikono, ambapo alipata nafasi ya kujifunza kuhusu sifa na ustadi wa kushona mavazi mbalimbali ya kitibet kwenye mikoa tofauti. Uzoefu kama huo ulimfanya awe hodari kwenye kila aina ya mavazi ya Tibet. Mwaka 2019, Losang Monlam alitambuliwa kuwa mrithi wa ujuzi wa kutengeneza ufundi wa ushonaji wa mavazi ya Lhasa. Mwaka 2022, alipewa pia jina la Mwalimu wa Sanaa na Ujuzi wa Lhasa.

Zaidi ya miaka 40 iliyopita, Losang Monlam amejitolea kurithisha ufundi. Mzee huyo mwenye umri wa miaka 60 amefundisha zaidi ya wanafunzi mia moja, na kujishughulisha katika kuandaa vitabu vya kiada na kuanzisha kanzidata ya mavazi ya Tibet. Kutokana na moyo wake, kwa sasa wabunifu vijana wanajaribu kuunganisha urithi wa utamaduni usioonekana na uzuri wa kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha