

Lugha Nyingine
Muundo mkuu wa Jengo la makao makuu ya Shirika la Ndege la Ethiopia lililojengwa na CCECC wakamilika
ADDIS ABABA, Agosti 18 (Xinhua) -- Jengo jipya la makao makuu ya Shirika la Ndege la Ethiopia, ambalo linaendelea kujengwa mjini Addis Ababa, sasa limeshuhudia kukamilika kwa ujenzi wa muundo wake mkuu.
Hafla ya kukamilisha muundo mkuu wa jengo hilo lenye kimo cha mita 45 ilifanyika Jumatatu, na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Shirika la Ndege la Ethiopia na Shirika la uhandisi wa ujenzi la China (CCECC).
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ndege la Ethiopia Bw. Mesfin Tasew, ameonyesha imani kuwa mradi huo utakamilika kama ilivyopangwa, ili kukidhi matakwa ya shirika la ndege ya muda mrefu.
Bw. Tasew amesema,“Tunataka jengo hili la makao makuu likamilike haraka iwezekanavyo, ni matarajio yetu makao makuu haya yakamilike kwa ubora wa hali ya juu.”
Mradi huu uliojengwa na kampuni ya CCECC kwenye eneo la ardhi la zaidi ya mita za mraba 33,560 una majengo sita tofauti yenye vifaa vingi, vikiwemo huduma za kibiashara, shirika na wateja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma