Ujenzi wa barabara inayojengwa na kampuni ya China waanza Mashariki mwa Ethiopia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 20, 2025
Ujenzi wa barabara inayojengwa na kampuni ya China waanza Mashariki mwa Ethiopia
Wageni wakihudhuria hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Mieso-Dire Dawa, Mashariki mwa Ethiopia, Agosti 19, 2025. (Xinhua/Han Xu)

ADDIS ABABA -- Ujenzi wa Barabara ya mwendokasi ya Mieso-Dire Dawa, ambayo ni mradi mkubwa wa miundombinu ndani ya Ukanda wa Usafiri wa Ethiopia na Djibouti, ulizinduliwa jana Jumanne huko Dire Dawa, mashariki mwa Ethiopia.

Kwenye hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa mradi huo, Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Temesgen Tiruneh amesema kujenga miundombinu ya barabara ni hatua muhimu ya kuwezesha maendeleo ya jamii na uchumi ya nchi.

Bw. Temesgen Tiruneh amesema zaidi ya asilimia 90 ya usafirishaji wa watu na bidhaa nchini Ethiopia unafanywa kupitia usafiri wa barabara. Barabara ya Mieso-Dire Dawa itakayounganisha mikoa ya Oromia na Somali na mji wa Dire Dawa, ina jukumu kubwa katika kuimarisha mwingiliano wa kiuchumi, kijamii na kisiasa kati ya mikoa hiyo na jamii.

Kandarasi wa mradi huo inayotekelezwa kwa pamoja na Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi ya China (CCECC) na Kampuni ya Ujenzi wa Barabara na Madaraja ya Sichuan, ina umbali wa kilomita 144 na itatekelezwa kwa vipindi viwili. Mradi mzima unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 48.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha