Xi Jinping asisitiza kujenga Xizang mpya ya kijamaa ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 21, 2025

Rais Xi Jinping wa China, akisikiliza ripoti za kazi kutoka kwa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Mkoa wa Xizang na serikali ya mkoa huo, na kutoa hotuba muhimu huko Lhasa, Mkoani Xizang, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

LHASA -- Rais Xi Jinping wa China ameutaka Mkoa Xizang kujenga Xizang mpya ya kijamaa yenye mshikamano, ustawi, ustaarabu, usawa na inayopendeza.

Rais Xi alisema hayo baada ya kusikiliza ripoti za kazi kutoka kwa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya mkoa wa Xizang na serikali ya mkoa huo. Rais Xi amesisitiza kuwa mkoa wa Xizang unapaswa kuhimiza kwa kasi maendeleo ya hali ya juu, na kuendelea kufanya juhudi katika kazi kuu nne za kuhakikisha utulivu, kusukuma mbele maendeleo, kulinda mazingira ya asili na kuimarisha usalama wa mpaka.

Rais Xi amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Xizang miaka 60 iliyopita, mkoa huo umepata maendeleo makubwa ya uchumi na jamii, na mabadiliko makubwa yametokea katika mkoa huo.

Rais Xi amesema kusimamia mkoa wa Xizang, kuhakikisha utulivu wake na kukuza ustawi wake, ni lazima kuanze kwa kudumisha utulivu wa kisiasa na kijamii, kuwa na mshikamano wa makabila na uhusiano wa kirafiki kati ya dini tofauti, na kutoa wito wa kuendeleza zaidi ujenzi wa jumuiya ya taifa la China.

Rais Xi pia amesisitiza haja ya kuhimiza mawasiliano ya pande mbilimbili kati ya mkoa wa Xizang na sehemu nyingine za China katika uchumi, utamaduni, na wafanyakazi, na kuifanya dini ya Kibuddha ya kitibet iendane na jamii ya kijamaa.

Rais Xi pia amesema kuwa Xizang inahitaji kuendeleza viwanda vyenye uwezo wa ushindani kwa kufuata hali yake halisi, hasa sekta ya kilimo na ufugaji, pamoja na sekta ya nishati safi. Amesema mkoa wa Xizang pia unapaswa kuendeleza kwa nguvu, utaratibu na ufanisi miradi mikubwa kama vile mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji katika maeneo ya chini ya Mto Yarlung Zangbo, na mradi wa Reli ya Sichuan-Xizang. Pia ametoa wito kwa mkoa huo kuhimiza uhifadhi wa ikolojia, na kufanya juhudi za uratibu za kupunguza utoaji wa hewa chafu, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kupanua maendeleo ya kijani, na kuendeleza ukuaji wa uchumi, ili kulinda “paa la dunia” na “mnara wa maji wa Asia.”

Rais pia amesisitiza kushikilia umuhimu wa uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China katika kazi husika za mkoa wa Xizang.

Rais Xi, ambaye ameongoza ujumbe mkuu, jumatano aliwasili Lhasa, mji mkuu wa mkoa wa Xizang, ili kushiriki kwenye shughuli za kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo, na Alhamis atahudhuria mkusanyiko mkubwa wa maadhimisho hayo mjini Lhasa.

Rais Xi Jinping wa China, akisikiliza ripoti za kazi kutoka kwa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Mkoa wa Xizang na serikali ya mkoa huo, na kutoa hotuba muhimu huko Lhasa, Mkoani Xizang, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China, akisikiliza ripoti za kazi kutoka kwa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Mkoa wa Xizang na serikali ya mkoa huo, na kutoa hotuba muhimu huko Lhasa, Mkoani Xizang, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha