

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ahudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Xizang
Rais Xi Jinping wa China, akiwapungia mkono watu wakati akihudhuria sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Xizang, mjini Lhasa, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
LHASA- Rais Xi Jinping wa China amehudhuria sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Xizang iliyofanyika jumatano jioni mjini Lhasa.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, aliungana na watu wa makabila yote huko Xizang kutazama tamasha la usiku la “Nyimbo za Shangwe za Uwanda wa Juu wenye Theluji.”
Rais Xi aliongoza ujumbe wa kamati kuu ya Chama kuwasili Lhasa mapema Jumatano kwa ajili ya shughuli za maadhimisho ya siku hiyo.
Rais Xi Jinping wa China, akiwapungia mkono watu wakati akihudhuria sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Mkoa unaojiendesha wa Xizang, mjini Lhasa, Agosti 20, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma