

Lugha Nyingine
UNEP na ICAO yazindua mradi wa kuondoa mapovu ya kuzima moto yenye sumu katika viwanja vya ndege vya Afrika
Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) yametangaza uzinduzi wa mradi wa kuimarisha uondoaji wa mapovu ya kuzima moto yenye sumu na badala yake kuweka njia mbadala salama katika viwanja vya ndege vya Afrika.
Ukipewa jina la "Kuimarisha Miundombinu kwa Uzimaji Moto wa Kuwajibika (FIRE)", mradi huo wenye thamani ya dola milioni 82.5 za Marekani utatekelezwa katika viwanja vya ndege vikubwa nchini Misri, Ethiopia, Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Viwanda na Uchumi cha UNEP, Sheila Aggarwal-Khan, ametaja mradi huo kama ni mpango muhimu ambao utaongeza uwezo wa nchi za Afrika kutokomeza uchafuzi wa mazingira unaodhuru ambao unapatikana katika minyororo ya usambazaji wa mapovu ya kuzima moto.
UNEP imesema utekelezaji wa mradi wa FIRE unatarajiwa kuondoa kwa njia salama tani 4,500 za nyenzo zilizochafuliwa na "per- and polyfluoroalkyl" (PFAS), kwenye magari ya zima moto na kuteketeza kwa usalama tani 130 za mapovu ya PFAS.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma