Mvua kubwa nchini Niger yasababisha vifo vya watu 47 na maelfu ya watu kuathirika

(CRI Online) Agosti 21, 2025

Kurugenzi Kuu ya Ulinzi wa Raia (DGPC) nchini Niger imesema mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka 2025 zimesababisha vifo vya watu 47 na wengine 70 kujeruhiwa kufikia Agosti 20.

Kwa mujibu wa DGPC, waathirika walikufa kutokana na kuporomoka kwa nyumba zao ambazo nyingi zilijengwa kwa udongo, au kutokana na kuzama. Mvua hizo pia zimeathiri kaya 7,754 na kuua mifugo 257.

Mnamo 2024, mvua kubwa zilizonyesha katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi zilisababisha vifo vya watu 396, kuathiri kaya 206,474, na kuharibu nyumba 158,767.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha