Kenya yazindua boti ya doria kuimarisha ulinzi wa wanyamapori

(CRI Online) Agosti 21, 2025

Shirika la Huduma za Wanyamapori nchini Kenya (KWS) jana jumatano limezindua boti ya kisasa ya doria kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi ikiwa ni katika juhudi za kuimarisha ulinzi wa Ziwa Turkana katika eneo la kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa KWS Erustus Kanga amewaambia wanahabari jijini Nairobi kwamba, boti hiyo, iliyolewa na wenzi wake, ina teknolojia za kisasa za rada na vifaa vya kutambua vitu vilivyomo chini ya maji kwa kufuata mawimbi ya sauti.

Amesema boti hiyo itaboresha usalama wa wahifadhi wa KWS huku ikiimarisha uwezo wao wa kulinda Ziwa Turkana kwa kuwezesha doria kufanyika kwa wakati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha