Mfuate Katibu Mkuu kusoma na kuelewa Ustaarabu wa China: Ustaarabu wa China wa zaidi ya miaka elfu moja kuakisi zama mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 21, 2025

Wakati tunapotazama sanamu hii ya mheshimiwa Confucius, mazungumzo kuhusu ustaarabu wa kuvuta muda wa miaka zaidi ya elfu moja yanaanza sasa.

Qufu, eneo linalojaa utamaduni wa wasomi wa Confucius, ambalo limeshuhudia mabadiliko na hali ya kung'ara ya ustaarabu wa China. Kutoka wazo lenye uwerevu kuhusu "maelewano ni ya thamani, waungwana hudumisha sifa zao kipekee wakati wa hali ya maafikiano" lililotolewa kwenye kitabu cha "Lun Yu", hadi matumaini yaliyoelezwa kwenye kitabu cha "Li Ji" kuhusu "Ulimwengu ni wa Umma", fikra ya wasomi wa Confucius imetukuza ustaarabu wa China, na pia imekuwa na ushawishi kwa watu wa nchi mbalibmali duniani.

Ustaarabu wa nchi mbalimbali unadumisha sifa pekee mbalimbali wakati wa hali ya maelewano, katika zama hizi zenye mafungamano ya pande nyingi, nuru ya akili za utamaduni wa wasomi wa Confucius inang'ara kwenye bahari ya ustaarabu wa nchi mbalimbali duniani. Kwa kukabiliwa na mabadiliko ambayo hayajatokea duniani katika miaka mia moja iliyopita, ustaarabu wa China unavuka wakati na nafasi ulimwenguni, ukifuata jumuishi na maafikiano na kupata mwitikio duniani. Utetezi wake ya "uwema na upendo", na "kutawala nchi kwa maadili" yamekuwa kama chemchemi ya akili kwa utatuzi wa masuala ya dunia nzima.

(Ungaji mkono na ufadhili ulitolewa na mtaji maalumu wa utangazaji mtandaoni wa China wa Mfuko wa Maendeleo ya Mtandao wa China.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha