

Lugha Nyingine
Baraza la Nishati la Afrika lafungua ofisi ya kimataifa huko Shanghai
Baraza la Nishati la Afrika (AEC) limefungua rasmi ofisi ya kimataifa mjini Shanghai, China, ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya serikali za Afrika, makampuni ya nishati na wenzao wa China.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AEC siku ya Alhamisi, ofisi ya Shanghai itaongozwa na Bieni Da, mwakilishi mkuu wa AEC nchini China, ambaye ana jukumu la kuhakikisha kuwa Baraza hilo linabeba jukumu muhimu katika kuunganisha biashara za China na taasisi za serikali na wadau wa Afrika.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa lengo lake liko wazi ambalo ni kuendesha ushirikiano wenye matokeo na wa muda mrefu katika sekta za kimkakati za uchumi, kuwezesha uwekezaji ambao utanufaisha pande zote mbili na unaokwenda sambamba na malengo ya maendeleo ya mabara yote mawili.
Baraza hilo limeongeza kuwa ofisi yake ya Shanghai itakuwa ni sehemu muhimu katika kuunganisha makampuni ya China na miradi ya Afrika, kuwezesha ushirikiano, na kuleta fursa za Afrika kwenye soko la China.
AEC, shirika la utetezi wa nishati lenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini, lilianzishwa mwaka 2018 likiwa na mamlaka ya kukuza uwekezaji endelevu na mbinu bora ndani ya sekta ya nishati barani Afrika.
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Michezo ya Dunia ya Chengdu | Sherehe ya Kufungwa kwa Michezo ya 12 ya Dunia yafanyika
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Mandhari ya Arxan yenye vivutio vingi vya utalii, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma