

Lugha Nyingine
China yaisaidia Senegal kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar ya 2026
China imeisaidia Senegal katika kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar 2026, tukio ambalo ni la kwanza la Olimpiki kufanyika katika bara la Afrika.
Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Asia ya Hangzhou imechangia zaidi ya vitu 13,000 kwa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Dakar. Aidha, China imewaalika wanariadha 96 wa Senegal wa michezo 12 kufanya mazoezi nchini China.
Katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Jumanne, Balozi wa China nchini Senegal Li Zhigang alisema, "Juhudi hizi zinaakisi kanuni za maendeleo ya kijani, kaboni chache, kuheshimiana na mshikamano wa ushirikiano."
Li pia alieleza imani yake kuwa Senegal itawasilisha Michezo bora ya Olimpiki ya Vijana kwa dunia. Alizihimiza pande zote kushirikiana ili kuhakikisha Michezo hiyo inafanikiwa na kuacha urithi wa kudumu kwa michezo ya vijana wa Afrika.
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Michezo ya Dunia ya Chengdu | Sherehe ya Kufungwa kwa Michezo ya 12 ya Dunia yafanyika
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Mandhari ya Arxan yenye vivutio vingi vya utalii, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma