AU yathibitisha kuunga mkono juhudi za kuleta utulivu nchini Somalia kufuatia vitisho vya kundi la al-Shabab

(CRI Online) Agosti 22, 2025

Mwakilishi maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) nchini Somalia ambaye pia ni mkuu wa Tume ya Kusaidia na Kuleta Utulivu ya Umoja wa Afrika (AUSSOM) El Hadji Ibrahima Diene amethibitisha dhamira yao ya kuimarisha amani, usalama na juhudi za kuleta utulivu nchini humo kufuatia vitisho vya al-Shabab.

Pia alipongeza operesheni za pamoja zinazoendelea za wanajeshi wa AU na Vikosi vya Usalama vya Somalia katika baadhi ya maeneo ya Somalia ili kukabiliana na vitisho vinavyoletwa na wanamgambo wa kundi hilo.

Diene alifanya ziara ya kwanza mjini Baidoa, mji mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi wiki hii, akisisitiza uungaji mkono wa AUSSOM kwa operesheni endelevu dhidi ya kundi la al-Shabab, ambalo limeimarisha uthabiti wake dhidi ya kampeni nyingi za kukabiliana na wapiganaji hao, na hivyo kuwa tishio kwa utulivu wa Somalia. Amepongeza ushirikiano mkubwa kati ya washirika wakuu wa kikanda na kimataifa katika juhudi za kuleta utulivu nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha