Uganda na Sudan Kusini zaahidi kufanya juhudi za pamoja katika kutatua hali ya wasiwasi mipakani

(CRI Online) Agosti 22, 2025

Jeshi la Uganda limesema majeshi ya Uganda na Sudan Kusini yamekubali kuimarisha ushirikiano, ili kutatua mapambano yanayotokea mara kwa mara mipakani, ambapo baadhi yao yamekuwa yakisababisha vifo.

Jeshi la Uganda Jumatano lilitoa taarifa likisema, maafisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Uganda walikutana na ujumbe wa Sudan Kusini huko Kampala, mji mkuu wa Uganda, ambapo walijadili changamoto za usalama zilizoko kwenye sehemu ya mpaka wa pamoja.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Uganda (UPDF) Muhoozi Kainerugaba, Kamanda wa vikosi vya nchi kavu vya UPDF Kayanja Muhanga alisema, pande mbili zina historia ndefu ya ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za pamoja.

Naye Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Sudan Kusini Dau Aturjong Nyuol alisisitiza tena kuwa Sudan Kusini inadhamiria kushirikiana na Uganda katika kutatua migogoro.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha