

Lugha Nyingine
Kipindi Kizuri cha Majira: Mwisho wa Joto
Hamjambo wote! Mimi ni Sisi, shabiki wa kutalii! Vipi, mmeona upepo wa asubuhi na jioni kwa sasa unakuwa mwepesi zaidi, na mwangaza mkali sana wa jua sasa umepungua? Hiyo ni kweli – sasa tumeingia katika kipindi cha Chushu, yaani kipindi cha joto kali kupungua, au kuagana na majira ya joto. Hivi sasa, niko katika eneo la Kanas, kaskazini magharibi mwa China katika Mkoa wa Xinjiang. Fuatana nami na upate uzoefu wa wakati huu tulivu ambapo muda wa mwisho wa majira ya joto unakutana na mwanzo wa majira ya mpukutiko.
Neno "Chushu", Chu lina maana ya "kwisha," likiashiria kuanza kuondoka polepole kwa joto la majira ya joto na kuwatuliza viumbe wote. Kwenye utamaduni wa jadi wa China, kuna "Chushu San Hou", yaani vipindi vitatu katika Chushu: Kwanza, mwewe wanaanza uwindaji wao wa majira ya mpukutiko ili kuhifadhi chakula kwa majira ya baridi; pili, hewa na dunia vinakuwa shwari; tatu, nafaka mashambani zinakomaa. Ishara hizi wazi za asili zinaonyesha mabadiliko ya majira na hekima ya jadi ya binadamu wanaishi pamoja na mazingira ya asili katika hali ya kupatana.
Katika mji wa Kanas, misitu ya birch ina majani yaliyofungamana kwenye mashina ya rangi ya fedha ya miti yake. Upepo unapovuma, majani madogo yenye umbo la moyo yanatoa sauti kana kwamba majira ya mpukutiko yanazungumza kwa sauti ya chini. Katika bonde la Mto Kanas, matabaka ya miti ya misonobari ni marefu kama miiba, na miiba yake laini huugawa mwanga wa jua na kuwa kama vipande vya dhahabu vinavyopeperuka. Ni msimu wa umande, matikiti yamekomaa, na kutokana na mwanga wa jua, maganda yake membamba yanahifadhi ladha tamu ndani yake. Nyasi za malisho zina rangi ya dhahabu iliyopauka, ng'ombe na kondoo wanarudi kwenye mazizi yao kwa furaha, na moshi kutoka kwenye nyumba za mbao za watu wa kabila la Watuva unafuka polepole. Hewa ya huko polepole inajaa harufu ya chai ya maziwa na siagi.
Wakati huo huo, Japan inaingia katika kipindi kati ya Liqiu (mwanzo wa majira ya mpukutiko) na Chushu, wakati huo watu wanatuma barua au kadi za salamu kwa marafiki na familia, wakiwatakia afya njema na kuwakumbusha kujitunza vizuri wakati majira yanapobadilika. Kutoka kwa vibanda vya mbao vya Kanas hadi salamu za majira ya joto huko Kyoto, kipindi cha Chushu kinatukumbusha kwamba mabadiliko ya majira ni lugha ya pamoja, ambayo inavuka mipaka na kuzungumza na binadamu wote.
“Upepo mwanana unapunguza joto la kiangazi; vitu vyote vinaingia kwenye majira mapya ya mpukutiko.” Kipindi cha Chushu ni safari kutoka majira ya joto kali kukamilika na kuelekea kwa majira ya mavuno ya mpukutiko. Hapa Kanas, safari hiyo inaelekea maeneo makubwa, yenye amani, na ya hali ya kimashairi. Vipi, dalili za majira ya mpukutiko zimeanza kukufikia huko uliko? Tuambie uzoefu wako kuhusu kipindi cha Chushu!
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Michezo ya Dunia ya Chengdu | Sherehe ya Kufungwa kwa Michezo ya 12 ya Dunia yafanyika
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Mandhari ya Arxan yenye vivutio vingi vya utalii, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma