Wang Yi akutana na mjumbe maalum wa Rais wa Korea Kusini Park Byung-seok

(CRI Online) Agosti 25, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi jana alikutana na Mjumbe Maalum wa Rais wa Korea Kusini Park Byung-seok mjini Beijing.

Wang Yi amesema kuwa baada ya serikali mpya ya Korea Kusini kuchukua madaraka, rais Xi Jinping na mwenzake Lee Jae-myung wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kufikia makubaliano muhimu ya kuinua ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Korea Kusini hadi ngazi ya juu na kuelekeza maendeleo ya baadaye ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Pande zote mbili zinapaswa kuzingatia matarajio ya awali ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia, kubaki na nia ya urafiki, kupanua maslahi ya pamoja, kuboresha hisia za umma, na kushughulikia ipasavyo masuala nyeti.

Park Byung-seok alimwomba Wang Yi kuwasilisha barua inayotoka kwa Rais Lee Jae-myung kwa Rais Xi Jinping, akieleza nia ya serikali mpya ya Korea Kusini kurejesha uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati kati ya Korea Kusini na China. Korea Kusini siku zote inaheshimu Kanuni ya kuwepo kwa China Moja na iko tayari kuendeleza uhusiano wa usawa na mataifa makubwa kama vile China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha