Iran yakataa kithabiti madai ya Marekani ya kutii masharti yake

(CRI Online) Agosti 25, 2025

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema, Marekani inajaribu kuilazimisha Iran kutii masharti yake kwa kuiwekea vizuizi.

Katika hotuba yake aliyoitoa jana jumapili mjini Tehran, Bw. Khamenei amesema, wale wanaounga mkono Iran kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani ili kutatua suala hilo hawana busara, na amesisitiza kuwa Iran itapinga kithabiti madai ya Marekani.

Pia amesema, Marekani inatarajia Iran kuitii, jambo linalowakasirisha sana watu wa Iran, ambao wako tayari kupambana kwa nguvu zake zote dhidi ya wale wanaounga mkono kitendo hicho cha Marekani.

Bw. Khamenei pia ameonya wapinzani wanaojaribu kutimiza malengo yao kwa kuzusha migawanyiko ndani ya Iran, na kutoa wito wa kuongeza juhudi katika kudumisha na kuimarisha umoja wa sasa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha