China yatoa wito kwa juhudi za jamii ya kimataifa kuondoa mvutano mashariki mwa DRC

(CRI Online) Agosti 25, 2025

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia kuondoa mvutano katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kurejesha amani ya kikanda.

Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi Sun amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuyataka makundi yote yenye silaha mashariki mwa DRC kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu, kuacha mara moja mapigano na kushiriki katika mchakato wa kusalimisha silaha, na kuunga mkono DRC katika kulinda maisha na mali za raia, wakiwemo raia wa kigeni.

Amesema China inapongeza juhudi za upatanishi zinazofanywa na Qatar zilizosaidia kusainiwa kwa Azimio la Kanuni kati ya serikali ya DRC na waasi wa M23, na kuongeza kuwa, wakati majadiliano hayo yanapoingia kwenye kipindi kigumu, China inatarajia Qatar itapendekeza makubaliano ya amani ya kudumu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha