RSF yashambulia hospitali na kuteka raia kutoka kwenye kambi kusini magharibi mwa Sudan

(CRI Online) Agosti 25, 2025

Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) cha nchini Sudan kimefanya mashambulio katika hospitali ya Kusini iliyoko mjini El Fasher, mji mkuu wa mkoa wa Darfur Kaskazini nchini Sudan na kuteka nyara raia wanane kutoka kwenye kambi iliyo jirani ya watu waliokimbia makazi yao.

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umesema katika taarifa yake kwamba, mizinga iliyorushwa na RSF ilishambulia hospitali hiyo jumamosi asubuhi na kujeruhi mhudumu mmoja wa afya na wagonjwa sita, wakiwemo mtoto na mama mjamzito.

Wakati huohuo, Chumba cha Dharura cha Abu Shouk, ambacho ni kundi la kujitolea, limesema wapiganaji wa RSF walivamia kambi ya watu wakikimbia makazi yao iliyoko kaskazini mwa mji wa El Fasher jumamosi iliyopita na kuteka raia wanane, huku zaidi ya watu 20 wanaoishi katika kambi hiyo hawajulikani walipo.

RSF haijatoa tamko lolote kuhusu matukio hayo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha