

Lugha Nyingine
Timu ya madaktari wa China yatoa matibabu kwa zaidi ya wagonjwa 7,000 nchini Zimbabwe
Timu ya 22 ya madaktari wa China nchini Zimbabwe imetoa matibabu kwa zaidi ya wagonjwa 7,000 wa huko.
Katika mazungumzo na Shirika la Habari la China Xinhua, timu hiyo imesema wataalamu 11 wa afya katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu ya neva na tiba ya mifupa, wamekuwa wakitoa ushauri wa bure kwa wagonjwa nchini Zimbabwe na wamefanya zaidi ya upasuaji 200 tangu walipoanza kutekeleza majukumu yao mwezi Machi mwaka huu.
Mtaalamu wa mifupa katika timu hiyo, Zhang Xiong amesema, baadhi ya wakazi kwenye maeneo ya vijijini wanashindwa kupata huduma nzuri ya matibabu, na kikosi hicho kimewafikia kwa kuwapa huduma ya matibabu.
China imepeleka timu 22 za madaktari nchini Zimbabwe tangu mwaka 1985, ambao wamechukua nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini humo.
Uwekaji wa nguzo za chuma kwenye Daraja la Mto Hanjiang la reli ya kasi ya Xi'an-Shiyan wakamilika
Michezo ya Dunia ya Chengdu | Sherehe ya Kufungwa kwa Michezo ya 12 ya Dunia yafanyika
Reli ya kasi China iliyoko kaskazini zaidi mwa China yafikisha miaka 10 tangu ilipoanzishwa
Mandhari ya Arxan yenye vivutio vingi vya utalii, Kaskazini mwa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma