Zaidi ya wapiganaji 35 wa kundi la ugaidi wauawa kwenye mashambulizi ya anga mpakani mwa Nigeria

(CRI Online) Agosti 25, 2025

Jeshi la anga la Nigeria limesema, zaidi ya wapiganaji 35 wa kundi la kigaidi wameuawa katika shambulio la anga lililofanywa na Jeshi hilo karibu na mpaka kati ya Nigeria na Cameroon jumamosi iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la anga la Nigeria imesema, wapiganaji hao walikuwa wanapanga kushambulia vikosi vya jeshi la Nigeria vilivyoko kwenye eneo la Kumche, jimbo la Borno.

Taarifa hiyo pia imesema, jeshi hilo lilishambulia vituo vinne vya wapiganaji hao kufuatia taarifa walizopokea kutoka kwa vyanzo vya kuaminika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha