Benin yafanya siku ya kimataifa ya kukumbuka biashara ya utumwa na kukomeshwa kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2025

OUIDAH – Watu wenye asili ya Afrika pamoja na viongozi wa kisiasa, watawala na wa kutoka sekta ya dini, Jumamosi iliyopita waliwakumbuka wahanga wa biashara ya utumwa huko Ouidah, mji wa kihistoria kusini mwa Benin, wakati wa siku ya Kimataifa ya Kukumbuka Biashara ya Utumwa na Kukomeshwa kwake.

Washiriki waliwakumbuka mababu zao kwa kutembea umbali wa takriban kilomita 2 kuanzia kwenye kituo cha zamani ya mnada wa watumwa cha Place aux Encheres, hadi kwenye Lango la Kutorodi Nyuma, mahali walipoondokea watumwa waliouzwa kwenda Amerika.

Waziri wa Utalii, Utamaduni na Sanaa wa Benin Jean-Michel Abimbola alisema siku hiyo ya kumbukumbu ya Agosti 23 kila mwaka, inawakumbusha watu wa Benin historia yenye uchungu ya mamilioni ya wanaume, wanawake na watoto kuuzwa.

Mtu mwenye asili ya Afrika kutoka Haiti Bw. Bertin Pedro, amekaribisha shughuli ya siku hiyo, akisema inasaidia kuimarisha uhusiano kati ya Benin na Waafrika wanaoishi nje ya Afrika, na kuongeza kuwa Benin imetangaza sheria inayotambua wahanga wa biashara ya utumwa wenye asili ya Afrika na kuwapa haki ya kupata uraia wa Benin.

Shughuli ya mwaka huu iliyofanyika chini ya kaulimbiu “Kumbukumbu, Uvumilivu na Wakati Ujao: Kuheshimu Wahanga, Kujenga Kesho” ambapo watafiti, watu kutoka sekta ya utamaduni na wawakilishi wa watu wanaoishi nje ya Afrika wenye asili ya Afrika wamekusanyika pamoja, ili kujadili namna ya kuhifadhi kumbukumbu na kuendeleza shughuli ya kumbukumbu ya siku hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha