Watu 20 wauawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel kwenye hospitali ya Gaza

(CRI Online) Agosti 26, 2025

Watu zaidi ya 20 wakiwemo waandishi wa habari watano wameuawa jana baada ya jeshi la Israel kushambulia mara mbili hospitali ya Nasser huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Chanzo cha usalama cha Ukanda wa Gaza kimeliambia Shirika la habari la China Xinhua kwamba, ndege za kivita za Israel zilishambulia kwanza hospitali ya Nasser na kisha kuwashambulia wafanyakazi wa afya waliokuwa wakifanya uokoaji.

Idara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetoa taarifa ikisema, miongoni mwa watu waliokufa ni pamoja na wafanyakazi wa matibabu, wagonjwa, waandishi wa habari, na wafanyakazi wa ulinzi wa raia, na wengine kadhaa kujeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha