Kampuni za China yaahidi uungaji mkono wa kiufundi kwa sekta ya afya ya Afrika Magharibi

(CRI Online) Agosti 26, 2025

Kampuzi za madawa za China zilizoshiriki maonyesho ya Sekta ya Afya na Madawa ya Afrika Magharibi na China yaliyomalizika hivi karibuni mjini Accra, Ghana, zimeahidi kuboresha utoaji wa huduma za afya katika kanda hiyo kwa teknolojia za kiuvumbuzi.

Maonyesho hayo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Kampuni ya China ya Afya ya Jamii ya Afrika Magharibi (HCOWA) iliyoko nchini Ghana, yalikutanisha zaidi ya kampuni 100 za huduma za afya kutoka China na Afrika Magharibi, kwa lengo la kuboresha matumizi ya Akili Bandia (AI) katika utambuzi wa kidaktari na kuimarisha uratibu kati ya China na nchi za Afrika Magharibi.

Katika maonyesho hayo, vifaa vingi vilionyeshwa ikiwa vifaa vya AI kwa Tiba ya Jadi ya China (TCM) na utambuzi wa jumla na mifumo ya upasuaji unaofanywa na robot.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha