Burundi yakamilisha mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2025 kwa kuchagua mabaraza ya vijiji na kata

(CRI Online) Agosti 26, 2025

Karibu Warundi milioni 6 walijitokeza kupiga kura jana jumatatu kuchagua wawakilishi wa mabaraza ya vijiji na kata, na kukamilisha mchakato wa uchaguzi wa nchi hiyo mwa mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya nchini humo, Prosper Ntahorwamiye amesema, Burundi ina vijiji na kata 3,044, na kila kimoja kinastahili kuwa wawakilishi watano, na kufanya jumla ya viti 15,220, na mgombea mwenye kura nyingi zaidi moja kwa moja anakuwa mwenyekiti wa kijiji ama kata.

Zoezi hilo lilifanyika kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 9 alasiri kwa saa za huko, huku viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais wa nchi hiyo Evariste Ndayishimiye wakipiga kura katika vijiji vyao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha