Kenya na ITU zazindua teknolojia ya mtandao wa kasi wa kielektroniki ili kuondoa pengo la kidijitali

(CRI Online) Agosti 26, 2025

Kenya na Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) ambalo ni shirika la kitaalamu la Umoja wa Mataifa, zimezindua zoezi la mtandao wa haraka wa kielektroniki linalolenga kuondoa pengo la kidijitali na kupanua upatikanaji wa mtandao wa kasi ya juu nchini humo.

Katibu mkuu wa Idara ya Utangazaji na Mawasiliano katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali nchini Kenya Stephen Isaboke, amewaambia wanahabari mjini Nairobi kwamba, nchi hiyo ina karibu watu milioni 46 wanaotumia simu za mtandao, na hatua hiyo itasaidia kutoa mtazamo unaoongozwa na takwimu kuelewa zaidi mandhari ya muundombinu wa mtandao na kutambua mapengo katika matumizi, ubora wa huduma, na gharama zake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha