Mlipuko wa kipindupindu wasababisha vifo vya watu zaidi ya 60 mashariki mwa Chad

(CRI Online) Agosti 26, 2025

Wizara ya Afya ya Chad imesema watu 63 wamekufa baada mlipuko wa kipindupindu kutokea mashariki mwa Chad.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo, jumla ya kesi 938 zinazoshukiwa zimerekodiwa, sampuli 52 zimechunguzwa, na kesi 39 zimethibitishwa mkoani Ouaddai, ambapo mlipuko huo umekuwa ukiendelea tangu mwezi Julai.

Mapema Jumatatu, Waziri wa Afya ya Umma nchini humo Abdelmadjid Abderahim alikutana na wahusika wa mamlaka ya afya huko Abeche, mji mkuu wa Mkoa wa Ouadai, kujadili mikakati ya kuzuia ugonjwa huo kuenea.

Abderahim amesema serikali imeongeza juhudi za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kuongeza uupatikanaji wa maji, usafi wa mazingira na wa watu binafsi.

Mamlaka hiyo pia imetoa wito wa kuchukua tahadhari na kufuata kwa makini hatua za usafi ili kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha