Wakimbizi 533 wa Rwanda warejea nyumbani kutoka DRC

(CRI Online) Agosti 26, 2025

Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya Rwanda imesema, wakimbizi 533 wa Rwanda jana wamerejea nchini humo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupitia kituo cha mpaka cha Grande Barrier katika Wilaya ya Rubavu, Mkoa wa Magharibi.

Katika taarifa yake, Wizara hiyo imesema, hatua hii imetimiza sehemu ya ahadi zilizotolewa wakati wa mkutano wa ngazi ya juu wa pande tatu uliofanyika tarehe 24 mwezi Julai huko Addis Ababa, Ethiopia, kati ya Rwanda, DRC na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha