Kampuni za biashara ya mtandaoni na za uwasilishaji bidhaa zawa na pilika nyingi katika Gulio la Siku ya "Double Eleven" kote China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 12, 2025
Kampuni za biashara ya mtandaoni na za uwasilishaji bidhaa zawa na pilika nyingi katika Gulio la Siku ya
Gari la kuwasilisha vifurushi linalojiendesha lenyewe likisafirisha vifurushi katika Mji wa Yangzhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Novemba 11, 2025. (Picha/cfp)

Jana Jumanne, Tarehe 11, mwezi wa 11 ilikuwa ni siku ya Gulio Kubwa la kila mwaka la Mtandaoni la China ambalo linajulikana zaidi kwa jina la Gulio la Siku ya Double Eleven. Kuanzia siku hiyo na siku kadhaa zijazo, kampuni za biashara ya mtandaoni na kampuni za kusambaza bidhaa kote nchini China zimekuwa zikitoa nguvu zote kufanya kazi katika kukabiliana na ongezeko kubwa la vifurushi vya bidhaa zilizonunuliwa wakati wa gulio hilo la Siku ya "Double Eleven."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha