Lugha Nyingine
Madaktari wa China watoa huduma za bure za afya kwa watoto katika makazi ya yatima Dar es Salaam (3)
![]() |
| Daktari wa timu ya madaktari wa China akitoa huduma za kliniki bila malipo kwenye kituo cha watoto yatima jijini Dar es Salaam, Tanzania, Desemba 13, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman) |
Vikundi vya madaktari wa China nchini Tanzania vimetoa huduma za matibabu ya bure kwa watoto wanaoishi kwenye makazi mawili ya watoto yatima mjini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mpango wa pamoja wa China-Afrika wa kuendeleza ustawi wa watoto yatima.
Kikundi cha 27 cha madaktari wa China Tanzania Bara na kikundi cha 35 cha madaktari wa China visiwani Zanzibar kiliendesha shughuli za kijamii katika vituo vya watoto yatima vya Zaidia na Ashura, ambapo madaktari 24 walifanya uchunguzi kamili wa afya na kutoa ushauri wa kitaalamu wa matibabu kusaidia ukuaji mzuri wa watoto hao.
Tukio hilo, lililopewa kaulimbiu "Kufariji Mioyo ya Watoto" limeandaliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania, na lilienda sambamba na utoaji wa michango ya chakula, mikoba ya shule, na vifaa vya kufundishia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




