Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina yachangia mahitaji kwa watoto wenye ulemavu nchini Zimbabwe (2)

(CRI Online) Desemba 16, 2025
Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina yachangia mahitaji kwa watoto wenye ulemavu nchini Zimbabwe
Wakazi wakipokea mahitaji kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Hunan, China wanaofanya shughuli zao nchini Zimbabwe huko Epworth, Harare, Zimbabwe, tarehe 14 Desemba 2025. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)

Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina nchini Zimbabwe imechangia shehena ya mahitaji ya kila siku kwa watoto wenye ulemavu huko Epworth, jumuiya ya wakazi iliyoko mjini Harare, Zimbabwe.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Hunan wanaofanya shughuli zao nchini Zimbabwe (HBAZ) Bw. Song Zhuolin kwenye hafla ya kugawa vitu hivyo siku ya Jumapili alisema kuwa mchango huo ni sehemu ya juhudi za uwajibikaji wa kijamii wa mashirika, na unawakilisha urafiki wa muda mrefu kati ya China na Zimbabwe.

“Tunahitaji kufanya wajibu wetu wa kijamii ili kusaidia kundi ambalo…. linahitaji uangalizi na huduma za ziada.” Bw. Song amesema.

Wakazi wa eneo la Epworth wameshukuru ishara hiyo ya wema kutoka kwa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina, wakisema kuwa michango hiyo itaboresha ustawi wa jamii.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha