Lugha Nyingine
Mwanamuziki abadilisha nyumba ya zamani kuwa klabu ya muziki huko Lijiang mkoani Yunnan, China
![]() |
| He Dehua akirekodi ili kuhifadhi milio ya ndege kwenye bustani katika mji wa kale wa Lijiang, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Januari 16, 2026. (Xinhua/Gao Yongwei) |
He Dehua mwenye umri wa miaka 51, na mkewe walikarabati nyumba yao ya zamani mwezi Oktoba mwaka 2025, na kuibadilisha kuwa klabu ya muziki inayoitwa "Wayfarers," (Wasafiri wa Njia) ambapo wanaweza kutoa simulizi zao binafsi kwa wasafiri na marafiki waliopotezana kwa muda mrefu.
Jina "Wayfarers" limetoka kwenye CD ambayo He aliitengeneza kwa ushirikiano na wengine. Alipata hamasa ya kubuni CD hiyo kutoka kwenye kumbukumbu zake za kuona wazee wa familia wakiacha maskani yao kwenda kufanya kazi kwa ajili ya kujipatia riziki. "Sote ni wasafiri wa njia katika maisha yetu wenyewe, lakini hatupaswi kusahau kutafuta hali halisi ya maisha na nafsi zetu," amesema.
He amekuwa ni mwanamuziki wa taaluma karibu kwa miongo mitatu tangu alipoenda kujifunza kupiga gitaa katika Mji wa Beijing mwaka 1997. Baada ya kurudi katika maskani yake ya Lijiang, alianza kujipa changamoto kwa kuvutia wageni katika mji huo wa zamani kwa kutumia muziki, nyimbo na milio ya mazingira ya asili.
Alianza kurekodi na kuhifadhi sauti na milio mwaka 2011, na amekusanya saa zaidi ya 200 za rekodi, ambazo zinajumuisha baadhi ya vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika, sauti katika maisha ya kawaida, na melodi zilizochezwa na wasanii wenyeji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




