Lugha Nyingine
Ujenzi wa minara mikuu ya daraja kubwa la Shiziyang katika Mkoa wa Guangdong, China wavuka mita 300
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2026
Ujenzi wa minara miwili mikuu ya daraja kubwa la Shiziyang, ambayo ni sehemu muhimu ya Njia ya Shiziyang katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, umevuka urefu wa kimo wa mita 300 jana Alhamisi.
Njia ya Shiziyang ni mradi mwingine mkubwa wa miundombinu baada ya Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao na Njia ya Kuunganisha Shenzhen na Zhongshan katika Eneo Kuu la Ghuba la Guangdong-Hong Kong-Macao kusini mwa China.
Daraja kuu hilo la Shiziyang ambalo ni sehemu muhimu ya mradi huo, lina urefu wa mita 2,180. Litakapokamilika, litafanya kazi yake muhimu katika maendeleo ya eneo la Mlango-Mto Zhujiang.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




